Alvimopani (Alvimopan), inayouzwa chini ya jina la chapa Entereg, ni dawa inayotumika kuharakisha kupona kutokana na ugonjwa wa ileus baada ya kupasuliwa kusiko kamili kwa sehemu ya matumbo kupitia njia ya anastomosisi ya upasuaji.[1] Dawa hii inaweza kutumika baada ya upasuaji wa utumbo mdogo au utumbo mkubwa.[2] Inachukuliwa kwa mdomo.[2]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kiungulia.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha mshtuko wa moyo na potasiamu ya chini.[1][2] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[3] Ni mpinzani wa kipokezi cha μ-opioid kinaychofanya kazi kwa pembeni.[2]
Alvimopani iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2008.[1] Nchini Marekani, dozi 15 za miligramu 12 hugharimu takriban Dola 2,900 kufikia mwaka wa 2022.[4]
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)