Kafara (kutoka neno la Kiarabu) ni kitu chochote kinachotolewa kuwa ni sadaka kwa Mwenyezi Mungu, kwa miungu, kwa pepo au kwa mizimu ili kuepuka balaa, madhara na maafa au kupata fadhili fulani. Mara nyingi damu ya kafara inatiwa maanani sana.
Kafara hutolewa zaidi katika matambiko, hasa kwa jamii nyingi za Afrika, ambapo watu huweza kuchinja wanyama kama sadaka kwa mizimu yao.
Hata hivyo wazo la kafara lipo pia katika dini mbalimbali, hadi kufikia hatua ya kuchinja watu kwa heshima ya miungu, hasa katika Mashariki ya Kati na barani Amerika.
Biblia ya Kiebrania inaonyesha kwamba tangu kale Mungu wa Israeli hakukubali kafara inayotolewa namna hiyo alipomzuia Abrahamu asimchinjie mwanae Isaka kama ilivyokuwa desturi ya makabila ya kandokando.
Katika Ukristo kafara hasa ni Yesu Kristo ambaye katika kifo na ufufuko wake alijitoa kadiri ya mapenzi ya Baba kwa wokovu wa watu wote[1].