Ketilo, C.R.S.A. (pia: Ketil, Chetillus, Ketillus, Keld, Kjeld,; Udani, 1100 hivi - Viborg, Udani, 27 Septemba 1150 hivi) alikuwa padri mwanajimbo ambaye alijunga na urekebisho wa Wakanoni akawa kielelezo cha umonaki, pamoja na kuwa na bidii kubwa kwa ajili ya seminari [1][2].
Papa Klementi III alimtangaza mtakatifu mwaka 1188[3].
Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki na Walutheri tarehe 11 Julai[4].