Kiabai-Sungai ni lugha ya Kiaustronesia nchini Malaysia inayozungumzwa na Waabai-Sungai. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kiabai-Sungai imehesabiwa kuwa watu 500 tu. Kwa vile Waabai-Sungai wengi wameacha lugha yao na kutumia lugha nyingine, lugha ya Kiabai-Sungai imekaribia kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiabai-Sungai iko katika kundi la Kiborneo-Kaskazini.