Kibahinemo ni lugha ya Kisepik nchini Papua Guinea Mpya inayozungumzwa na Wabahinemo. Mwaka wa 1998 idadi ya wasemaji wa Kibahinemo imehesabiwa kuwa watu 550. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibahinemo iko katika kundi la “Sepik Hill”.