Kibamenyam ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Wabamenyam. Mwaka wa 1994 idadi ya wasemaji wa Kibamenyam imehesabiwa kuwa watu 4000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibamenyam iko katika kundi la Grassfields ambalo linafanana na lugha za Kibantu.