Kibardi (au Kibaard) ni lugha ya asili nchini Australia inayozungumzwa na Wabardi katika jimbo la Australia ya Magharibi. Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kibardi ilihesabiwa kuwa watu 160, na lugha iko hatarini mwa kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibardi kiko katika kundi la Kinyulnyulan.