Kibentong (pia Kidentong) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabentong kwenye kisiwa cha Sulawesi. Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kibentong imehesabiwa kuwa watu 25,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibentong iko katika kundi la Kisulawesi-Kusini.