Kiberakou ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Chad inayozungumzwa na Waberakou. Mwaka wa 1995 idadi ya wasemaji wa Kiberakou imehesabiwa kuwa watu wawili tu. Kwa hiyo inawezekana kuwa lugha ya Kiberakou imeshatoweka kabisa sasa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiberakou iko katika kundi la Kibongo-Bagirmi.