Kibirri ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati inayozungumzwa na Wabirri. Mwaka wa 1996 idadi ya wasemaji wa Kibirri imehesabiwa kuwa watu 200 tu. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibirri iko katika kundi la Kibongo-Bagirmi.