Kibobongko ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabobongko kwenye visiwa vya Togian na Batu Daka. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kibobongko imehesabiwa kuwa watu 1500. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibobongko iko katika kundi la Kicelebiki.