Kiboma ni lugha ya Kibantu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayozungumzwa na Waboma. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kiboma imehesabiwa kuwa watu 20,500. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kiboma iko katika kundi la B80.