Kibuso ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Chad inayozungumzwa na Wabuso. Mwaka wa 1971 idadi ya wasemaji wa Kibuso imehesabiwa kuwa watu 40 tu. Kwa hiyo inawezekana kuwa lugha imeshatoweka kabisa hadi sasa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibuso iko katika kundi la Kichadiki.