Kibusoa ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabusoa kwenye kisiwa cha Buton. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kibusoa imehesabiwa kuwa watu 2300. Kwa vile Wabusoa wameanza kuacha lugha yao, Kibusoa imekaribia kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibusoa iko katika kundi la Kicelebiki.