Kibutuanon ni lugha ya Kiaustronesia nchini Ufilipino inayozungumzwa na Wabutuanon. Mwaka wa 1990 idadi ya wasemaji wa Kibutuanon imehesabiwa kuwa watu 34,500. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibutuanon iko katika kundi la Kifilipino.