Kiefate-Kusini ni lugha ya Kiaustronesia nchini Vanuatu inayozungumzwa na Waefate kwenye kisiwa cha Efate. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kiefate-Kusini imehesabiwa kuwa watu 6000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiefate-Kusini iko katika kundi la Kioseaniki.