Kihonda

Kata ya Kihonda
Majiranukta: 6°49′12″S 37°38′36″E / 6.82000°S 37.64333°E / -6.82000; 37.64333
Nchi Tanzania
Mkoa Morogoro
Wilaya Morogoro Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 35,579

Kihonda ni kata ya Wilaya ya Morogoro Mjini katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67114.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 35,579 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 44,424 waishio humo.[2] Hivyo ni kata kubwa zaidi katika Wilaya hiyo yote.

Inapatikana kwenye barabara inayoelekea Dodoma.

Kata ya Kihonda ina shule nyingi sana.

Kata ina tatizo la maji, ambalo limekuwa kero kwa wakazi, hasa kwa wale wa Kihonda Kwa Chambo.

Kata ilikuwa ikisumbuliwa na uhalifu, kama vile ujambazi na wizi. Hapo wanakata wakaitisha kikao ili kuzuia uhalifu huo wakapata njia ya kwamba usiku kuwe na walinzi waitwao sungusungu. Ingawa walikamatwa wezi, ulinzi uliendelea mpaka wezi walipotokomea.

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. http://www.meac.go.tz/sites/default/files/Statistics/Tanzania%20Population%20Census%202012.pdf Ilihifadhiwa 2 Januari 2004 kwenye Wayback Machine. Wilaya ya Morogoro Mjini - Mkoa wa Morogoro

Kihonda

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne