Kiiceve-Maci ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Waiceve-Maci. Mwaka wa 1990 idadi ya wasemaji wa Kiiceve-Maci imehesabiwa kuwa watu 7000. Pia kuna wasemaji 5000 nchini Nigeria. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiiceve-Maci iko katika kundi la Kitivoidi ambalo linafanana na lugha za Kibantu.