Kiifo ilikuwa lugha ya Kiaustronesia nchini Vanuatu iliyozungumzwa na Waifo kwenye kisiwa cha Erromanga. Msemaji wa Kiifo wa mwisho alifariki mwaka wa 1954, yaani lugha imetoweka kabisa sasa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiifo iko katika kundi la Kioseaniki.