Kiinonhan ni lugha ya Kiaustronesia nchini Ufilipino inayozungumzwa na Wainonhan kwenye kisiwa cha Tablas. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kiinonhan imehesabiwa kuwa watu 85,800. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiinonhan iko katika kundi la Kifilipino.