Kijumjum ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Sudan na Sudan Kusini inayozungumzwa na Wajumjum. Wataalamu wengine huiangalia kuwa lahaja ya Kimabaan. Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kijumjum imehesabiwa kuwa watu 25,000, yaani nchini Sudan na Sudan Kusini pamoja. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kijumjum iko katika kundi la Kinilotiki.