Kikagayanen ni lugha ya Kiaustronesia nchini Ufilipino inayozungumzwa na Wakagayanen kwenye kisiwa cha Cagayan. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kikagayanen imehesabiwa kuwa watu 30,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikagayanen iko katika kundi la Kifilipino.