Kikaluli ni lugha ya Kivuka-Guinea Mpya nchini Papua Guinea Mpya inayozungumzwa na Wakaluli. Mwaka wa 1994 idadi ya wasemaji wa Kikaluli imehesabiwa kuwa watu 2500. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikaluli iko katika kundi la Kibosavi.