Kikaonde ni lugha ya Kibantu nchini Zambia inayozungumzwa na Wakaonde. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kikaonde imehesabiwa kuwa watu 207,000. Pia kuna wasemaji 36,000 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kikaonde iko katika kundi la L40.