Kikaramojong ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Uganda inayozungumzwa na Wakaramojong. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kikaramojong ilihesabiwa kuwa watu 260,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikaramojong kiko katika kundi la Kinilotiki.