Kikaure ni lugha ya Kipapua nchini Indonesia inayozungumzwa na Wakaure. Mwaka wa 1995 idadi ya wasemaji wa Kikaure imehesabiwa kuwa watu 450, na lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kikaure iko katika kundi lake lenyewe la Kikaure.