Kilese ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayozungumzwa na Walese. Mwaka wa 1991 idadi ya wasemaji wa Kilese imehesabiwa kuwa watu 50,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kilese iko katika kundi la Kisudani cha Kati.