Kilevuka (pia Kipainara) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Walevuka kwenye kisiwa cha Lembata. Mwaka wa 2008 idadi ya wasemaji wa Kilevuka imehesabiwa kuwa watu 4000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kilevuka iko katika kundi la Kibima-Lembata.