Kilun-Bawang (pia Kilun-Daya) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia na Malaysia inayozungumzwa na Walun-Bawang kwenye kisiwa cha Kalimantan. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kilun-Bawang nchini Indonesia imehesabiwa kuwa watu 23,000. Na mwaka wa 1982 idadi ya wasemaji wa Kilun-Bawang nchini Malaysia imehesabiwa kuwa watu 24,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kilun-Bawang iko katika kundi la Kiborneo-Kaskazini.