Kimomuna ni lugha ya Kipapua nchini Indonesia inayozungumzwa na Wamomuna. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kimomuna imehesabiwa kuwa watu 2000. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kimomuna iko katika kundi la Kisomahai. Wengine huiangalia kuwa lugha ileile ya Kimomina.