Kingangam ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Togo na Benin inayozungumzwa na Wangangam. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kingangam nchini Togo imehesabiwa kuwa watu 46,000. Pia kuna wasemaji 20,000 nchini Benin. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kingangam iko katika kundi la Kigur.