Kipaku ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wapaku kwenye kisiwa cha Kalimantan. Mwaka wa 2003 idadi ya wasemaji wa Kipaku imehesabiwa kuwa watu 3500 lakini idadi imepungua tena tangu pale. Kuna Wapaku wachache tu ambao hutumia lugha ya Kipaku kama lugha yao ya kwanza, maana yake Kipaku iko njiani pa kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kipaku iko katika kundi la Kibarito.