Kiparenga (au Kigorum) ni lugha ya Kiaustro-Asiatiki nchini Uhindi inayozungumzwa na Waparenga. Mwaka wa 2001 idadi ya Waparenga imehesabiwa kuwa watu 12,600 lakini wengi wao hutumia Kioriya ya Adivasi kama lugha yao badala ya Kiparenga. Kwa hiyo, lugha ya Kiparenga iko karibu na kutoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kiparenga iko katika kundi la Kimunda.