Kipular ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Guinea, Sierra Leone, Senegal na Mali inayozungumzwa na Wapular. Isichanganywe na Kipulaar ambacho huzungumzwa hasa nchini Senegal, Gambia na Mauretania. Mwaka wa 1991 idadi ya wasemaji wa Kipular nchini Guinea imehesabiwa kuwa watu zaidi ya milioni mbili na nusu. Pia kuna wasemaji 178,000 nchini Sierra Leone, 150,000 nchini Senegal na 50,000 nchini Mali (1991). Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kipular iko katika kundi la Kiatlantiki.