Kirajbanshi ni lugha ya Kihindi-Kiulaya nchini Nepal inayozungumzwa na Warajbanshi. Mwaka wa 2011 idadi ya wasemaji wa Kirajbanshi imehesabiwa kuwa watu 143,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kirajbanshi iko katika kundi la Kiaryan. Wengine huiangalia kama lahaja ya Kirangpuri nchini Uhindi na Bangladesh.