Kisawai ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wasawai kwenye kisiwa cha Halmahera. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kisawai imehesabiwa kuwa watu 12,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kisawai iko katika kundi la Kihalmahera-Kusini.