Kisekak (pia Kilonchong) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wasekak kwenye kisiwa cha Bangka. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kisekak imehesabiwa kuwa watu 420 tu, maana yake lugha iko hatarini mwa kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kisekak iko katika kundi la Kimalayiki.