Kizangwal ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Nigeria inayozungumzwa na Wazangwal. Mwaka wa 1993 idadi ya wasemaji wa Kizangwal imehesabiwa kuwa watu 100 tu, yaani lugha iko katika hatari ya kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kizangwal iko katika kundi la Kichadiki.