Liseri (alifariki 540 hivi) alikuwa Askofu wa Couserans (Ufaransa) kwa miaka mingi na kwa sala zake alizuia mji huo usivamiwe na Wavisigothi[1].
Alitokea Hispania na kuwa mfuasi wa Fausto wa Riez[2].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Agosti.[3]
{{cite book}}
: CS1 maint: unrecognized language (link)