Nabore

Mt. Nabore katika mozaiki ya kanisa la Mt. Vikta Mwafrika mjini Milano, Italia.

Nabore alikuwa askari Mkristo kutoka Mauretania (katika Algeria ya leo).

Tarehe 12 Julai 303 BK, huko Lodi Vecchio (Lombardia) aliuawa pamoja na Waberberi wenzake Vikta na Feliche[1]

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na wengineo kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa siku ya kifodini chake[2][3].

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/62000
  2. Martyrologium Romanum
  3. http://catholicsaints.info/saint-nabor-of-milan/

Nabore

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne