Nyuki-kekeo | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Coelioxys froggatti
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Familia 3 zenye nyuki-kekeo na jenasi 8 katika Afrika ya Mashariki:
|
Nyuki-kekeo (kutoka kwa Kiing. cuckoo bees) ni nyuki waliotaga mayai yao katika viota vya nyuki wengine, kama vile kekeo hufanyia ndege wengine. Kuna makundi mbalimbali ya nyuki-kekeo. Jenasi iliyoenea zaidi na kuwa na spishi nyingi barani Afrika ni Coelioxys ya familia Megachilidae yenye spishi 21 katika Afrika ya Mashariki. Jenasi nyingine ya familia hii, Euaspis, ina spishi chache, ambazo moja tu imerekodiwa kutoka Afrika ya Mashariki. Makundi mengine hutokea katika familia Apidae, muhimu zaidi duniani kote ikiwa nusufamilia Nomadinae yenye spishi 14 katika Afrika ya Mashariki. Kabila Melectini ina spishi 20 za Afrika ya Mashariki katika jenasi Afromelecta na Thyreus. Makabila mengine nne zilizo na nyuki-kekeo hazipatikani Afrika (Bombini, Ericrocidini, Euglossini na Isepeolini). Katika familia Halictidae jenasi Sphecodes ina spishi 6 za nyuki-kekeo katika Afrika ya Mashariki.