Olegari (kwa Kikatalunya: Oleguer Bonestruga; Barcelona, 1060 hivi - Barcelona, 1137) alikuwa askofu wa Barcelona na wa Tarragona, nchini Hispania, kuanzia mwaka 1116.
Kabla ya hapo alikuwa mkanoni mwanajimbo, halafu Mwaugustino, halafu abati wa monasteri. Alipochaguliwa kuwa askofu alikataa cheo hicho mpaka alipoagizwa na Papa Paskali II[1].
Tangu zamani anaheshimiwa kama mtakatifu. Heshima hiyo ilithibitishwa na Papa tarehe 18 Mei 1675.