Ositha (pia:Osgyth, Osyth, Sythe na Othith; alifariki 700 hivi) alikuwa binti wa ukoo wa kifalme wa Mercia.
Mzaliwa wa Quarrendon, Buckinghamshire alilelewa katika monasteri hukon Warwickshire chini ya mtakatifu Modwen akatamani kuwa abesi, lakini alilazimishwa na baba yake Mpagani kuolewa na mfalme Sighere wa Essex akamzalia mtoto wa kiume.
Baadaye akaweka nadhiri za kimonaki akaanzisha monasteri huko Chich, Essex, akaiongoza hadi kifo chake ambacho kilihesabiwa kama kifodini[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waanglikana kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimisha tarehe 7 Oktoba.