Plekelmi (pia: Plechelm, Pleghelm, Plechelmus; Ireland au Britania, karne ya 7 – Roermond, Uholanzi ya leo, 730 hivi) alikuwa mmonaki askofu maarufu kwa umisionari wake kati ya Wafrisia[1].
Pamoja na wenzake Viro askofu na Odgeri shemasi alianzisha monasteri alimofariki[2].
Alitangazwa na Papa Agapeto II kuwa mtakatifu mwaka 950 hivi.