Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Rizavu

Rizavu ilikuwa eneo katika koloni za Uingereza ambako wazalendo waliruhusiwa kuishi kufuatana na mila na desturi zao.

Katika mengi sheria zilizotawala maisha ya koloni zilikuwa sheria za Uingereza (pamoja na sheria za kimahali). Katika koloni zao Waingereza walipendelea muundo wa utawala kupitia viongozi wazalendo kwenye ngazi za chini. Muundo huu ulitumiwa hata kwa maeneo makubwa katika nchi lindwa (protectorates) za Uingereza.

Hasa katika koloni ambako Waingereza walitegemea kuongeza idadi ya walowezi Wazungu rizavu ilikuwa nchi ya pekee ambako wazalendo waliruhusiwa kuwa na mali ya ardhi.


Previous Page Next Page