Sosyo (Miseno, mkoa wa Campania, leo nchini Italia 275 - Pozzuoli, Campania, 305) alikuwa shemasi aliyeuawa pamoja na askofu Januari na wenzake.
Papa Simako alisimulia kwamba Sosio, akitamani kumuepusha na kifo askofu wake huyo, alijikuta anaungana naye katika kifodini, akipata kwa gharama ileile utukufu uleule wa kwake.[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa hasa tarehe 23 Septemba[2].