Wamadi ni kabila la watu wanaoishi kaskazini mwa Uganda (Wilaya ya Adjumani na Wilaya ya Moyo) na kusini mwa Sudan Kusini.
Wanakadiriwa kuwa zaidi ya 400,000.
Lugha ya wengi wao ni Kimadi (Madi ti), mojawapo kati ya lugha za Kisudani na leo dini yao ni Ukristo, lakini pia Uislamu.