Wanyaturu (au Waturu; wao hupendelea kuitwa Arimi, yaani watu wa Rimi [1]) ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Mkoa wa Singida.
Lugha yao ni Kinyaturu, ambayo kwa sehemu ina matamshi ya Kibantu, ingawa ina fonimu nyingi za Kikushi. Hii inaweza kuwa kwa sababu ya muingiliano wa karibu na majirani zao Wanyatunzu (watu wa kaskazini magharibi) na Wanyiramba wa maeneo ya jirani ambao ni Bantu asili.
Wana utani na Wanyiramba na Wairaqw.
Asilimia kubwa ya Wanyaturu wa sasa ni weupe: hii ni kutokana na miingiliano yao na Waarabu na kupelekea kuzaliwa machotara wengi.
Wanyaturu wengi ni Waislamu na Wakristo, kwa jumla ni wachamungu kwani ni watu wanaojua kuishika dini vizuri na kupenda ibada.
Wanyaturu wanajua sana kulinda ardhi yao kwani ni vigumu Mnyaturu kuuza ardhi yake kwa mtu ambaye si Mnyaturu.