Airbus SAS ni kampuni kubwa ya kutengeneza eropleni katika Ulaya na moja ya makampuni makubwa duniani katika fani hii.
Kwa jumla imeajiri watu 50,000 katika nchi mbalimbali na hasa katika viwanda vyake huko Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Hispania.
Tangu mwaka 2001 Airbus imekuwa kampuni inayotengeneza ndege za kusafirisha abiria nyingi duniani. Ni hasa aina mbalimbali kama vile Airbus A300, Airbus A310 au Airbus A320. Tangu mwaka 2007 Airbus A380 ni ndege kubwa kabisa ya kubeba abiria duniani.