Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.
Ala ya muziki
Ala ya muziki ni kifaa kinachotoa sauti zinazotumiwa katika muziki. Kila ala ya muziki inatoa mitetemo katika hewa inayoendelea kusambaa na kupokewa na masikio kama sauti.
Kimsingi kila kitu kinachotoa sauti kinaweza kutumiwa kama ala ya muziki, lakini kwa kawaida jina hili linatumika kwa vitu vilivyotengenezwa hasa kwa shabaha hii. Wakati mwingine hata sauti ya binadamu inatajwa kama ala ya muziki.
Kuna aina nyingi za ala za muziki. Mara nyingi zinaainishwa na kutajwa kutokana na mbinu zake za kutoa sauti:
ala za nyuzi (ing. chordophone) kama vile gitaa, fidla, selo, zeze au piano; hapa uzi au waya iliyokazwa inapigwa au kuchuliwa hivyo inaanza kutetema
ala za utando (ing. membranophone) kama vile ngoma, tari, hapa utando inatoa mitetemo ikipigwa
ala za hewa (ing. aerophone) ambako nguzo ya hewa inatetemewa, mfano filimbi, kinanda cha filimbi, zumari, kipenga, baragumu, au tarumbeta. Katika kundi hili hewa inaweza kupititishwa kwenye kona kali kama kwa filimbi, au kwa kipande cha tete inayotetema katika mwendo wa hewa, au kwa kutumia midomo kama asili ya mitetemo kama kwenye tarumbeta.